Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2020

UMUHIMU MKUBWA USIOUJUA WA #MAZOEZI.

 Na brightermango.      Mazoezi ni ziada ya kile unachofanya kwa muda mfupi kila siku ili kuuchosha mwili wako, kwa hiyo ukitaka kuyaona matokeo ya mazozoezi unayoyafanya basi ni muhimu sana uwe unazidisha kila wakati mahali ulipoishia kufanya siku iliyopita. Hello?  mimi niko poa na ninamshkuru Mungu kwa uhai wangu. Ni matumaini yangu KUWA NA WEWE NI MZIMA... Ni muda sasa umekuwa ukifanya mazoezi na cha ajabu unajisifia huwa unafanya mazoezi, wakati kila siku unarudia idadi ile ile ya mazoezi, kitu ambacho hakikusaidii chochote, kwani ulichofanya ni sawa na kazi yako unayofanya kujiingizia kipato chako cha kila siku. Hebu sikiliza kwa umakini kwa kile ninachotaka kukwambia,  FAIDA ZA MAZOEZI KWA UJUMLA.  Faida zifuatazo zinaambatana na mwili wenye mazoezi;  1. HUJENGA KINGA IMARA YA MWILI. Kadri unavyofanya mazoezi ndivyo unavyoruhusu utengenezwaji mwingi wa chembe nyeupe za seli za damu ambazo ndio walinzi wakubwa wa mwili wetu, na kwa wakati fulani tumesaidika kwa ulinzi huu hata ka