Skip to main content

UMUHIMU MKUBWA USIOUJUA WA #MAZOEZI.

 Na brightermango. 

    Mazoezi ni ziada ya kile unachofanya kwa muda mfupi kila siku ili kuuchosha mwili wako, kwa hiyo ukitaka kuyaona matokeo ya mazozoezi unayoyafanya basi ni muhimu sana uwe unazidisha kila wakati mahali ulipoishia kufanya siku iliyopita.

Hello? 
mimi niko poa na ninamshkuru Mungu kwa uhai wangu. Ni matumaini yangu KUWA NA WEWE NI MZIMA...
Ni muda sasa umekuwa ukifanya mazoezi na cha ajabu unajisifia huwa unafanya mazoezi, wakati kila siku unarudia idadi ile ile ya mazoezi, kitu ambacho hakikusaidii chochote, kwani ulichofanya ni sawa na kazi yako unayofanya kujiingizia kipato chako cha kila siku.

Hebu sikiliza kwa umakini kwa kile ninachotaka kukwambia, 

FAIDA ZA MAZOEZI KWA UJUMLA.
 Faida zifuatazo zinaambatana na mwili wenye mazoezi;

 1. HUJENGA KINGA IMARA YA MWILI.
Kadri unavyofanya mazoezi ndivyo unavyoruhusu utengenezwaji mwingi wa chembe nyeupe za seli za damu ambazo ndio walinzi wakubwa wa mwili wetu, na kwa wakati fulani tumesaidika kwa ulinzi huu hata kama tulikuwa mahali pabaya kiasi cha kutojua kwa sababu ya ulinzi huu.

2. HUONGEZA UWEZO WA KUPUMUA.
Damu ya mwanadamu ni tishu na iko na viini seli vyake vitatu, lakini sasa hivi tunaenda kuangalia kiini mojawapo cha seli nyekundu ya damu, hii hubeba hewa ya oksijeni kutoka kwenye alveoli karibu na mapafu na hivyo kuboresha upatikanaji wa hewa ya oksijeni, kurahisisha upatikanaji wa nishati mwili na pia hurahisisha upumuaji wa watu wasiopumua vizuri.

3. MAZOEZI YANAJENGA SIHA NJEMA.
Tunapofanya mazoezi kiujumla tunalazimisha kujichosha tukiwa na lengo la kuweka sawa miili yetu, hivyo mabadiliko ya mwili tunayokuwa tunayatafuta ndio tunaita "siha", kwahiyo kubaki kwenye siha njema ni jukumu la dhati la kwetu kuhakikisha tunafanya mazoezi kila siku. Kile unachokiona ni siha njema, hutokana na vile unavyolazimisha misuri na mikano ya mwili wako ili kuujenga mwili wako.

4. MAZOEZI HUYEYUSHA MAFUTA MWILINI.
Endapo una tatizo la kiafya ambalo linaambatana na uwepo wa mafuta kwenye mirija ya damu, au mishipa ya damu, ufanyaji wa mazoezi ni muhimu kwani unayeyusha mafuta kwenye mirija ya damu na kukurejeshea namna njema ya mzunguko wako wa damu. mojawapo ya faida kubwa ya wewe kupata mzunguko bora wa damu ni kuondoa kichwa kugonga, kuondoa uzembe wa kufikiri na kukuchangamsha wakati wa jua kali au mchana.

5. MAZOEZI NI TIBA YA JUMLA.

Kuna vitu havitibiwi na dawa, na kwa kawaida inaelekea vinatambulika kama sio magonjwa... mojawapo ya magonjwa ni ..
Msongo wa mawazo, Kupata homa, mwili kuuma na uchovu, aleji ya mwili.

Niko naona faida nyingi lakini hizi TANO zitakuwa msaada wako kwa siku zako za usoni.





'We believe, life is only a gift that expires and success in anything we have is not ours, its for human kind and so our wisdom'' -Gwemela

Comments

Popular posts from this blog

SIRI|| KUFANIKIWA NI KUSUBIRI.

 Na brightermango. VIPI UMEJARIBU KILA KITU LAKINI  BADO TU UNAKWAMA? Hapana, hujajaribu kila kitu, JE? umejaribu kuendelea kusubiri zaidi. Kuna wakati tunatamani mambo yaliyo juu ya upeo wetu, na tukishauriwa mara nyingi tunagundua hatukupaswa kuyatamani na badala yake kutafuta uwezo kwanza wa kuwa pale kama wahusika, yaani ninachokisema ni kwamba; "TUNAPOTAMANI KUWA KWENYE SHEREHE YA KUHITIMU ELIMU YA CHUO, BASI TULIPASWA KUWA WANACHUO AU WAHUSIKA KWA NAMNA FULANI" au "HUWEZI TUNUKIWA MEDANI KAMA HUKUSHIRIKI MASHINDANO HUSIKA" Basi ndivyo ilivyo kwenye maisha, Yaani ukiyahitaji mambo fulani hapa duniani, jitahidi ujue vigezo vyake ili na wewe uweze kuwa kama vigezo vinavyokutaka. Sasa kwenye hili letu la kujaribu kila kitu lakini bado husogei, Je? Ndio haiwezekani tena wewe kuinuka juu na kufanya mambo yako kwa mafakio? Nifuate kuna kitu leo nitakufunza,... NGOJA TUCHIMBE BUSARA ZA MABABU. Kutoka kwenye kitabu cha THE LIFE, Kinachohusika na uandishi wa...

DID YOU EVER ASK YOURSELF ABOUT THIS BEFORE ? THAT FATE RELY ON YOU CHOICES?

Well it may sound bit rude to ask a kind of such question, but indeed we need to the answer to be assured of one thing, and that is our mind safety on everything that we daily do. some of the other tend to happen as coincidences but other are bit difficult to decide whether they have happened just as the coincidence and therefore put us into worry. you know what? in Africa, people with just such curiosity goes to witch doctors that they may know what holds their future. with the false telling and sometimes enmity creation between the family members is being planted by these witch-doctors.   Which is why people tend to be brought around the corner with nothing related to the future that they were after, unknowingly they become servants to the blasphemer(devil), hahahah um, it is sometime big thing to come up with the idea of fate that holds the future, it is because of what fate holds unto us and the total surrounding that we are in, that we grow curiosity toward future.   ...

IS IT TRUE THAT "LEARNING IS ALL ABOUT REHERSAL''

TAP down bellow in the comment place and share your opinion over this topic of discussion.