Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2020

JINSI WOTE TULIVYO WASIOHAKI...LAKINI TUNAMUHUKUMU MWIZI.

 HIVI UNAFAHAMU KUWA❓ "HATA MWIZI UNAYEMKAMATA BAADA YA KUKUIBIA, NA YEYE PIA ALIKUWA AKIKAMILISHA FURAHA YAKE, SEMA TOFAUTI NA WEWE, YEYE HAWEZI KUVUMILIA MAUMIVU NA KUKUSANYA KIDOGO KIDOGO NA KWAHIVO ANATUMIA NGUVU KUBWA AKILI MBAYA ILI KUPATA PESA AU MALI NYINGI KWA WAKATI MFUPI BILA YA UCHOVU AU MAUMIVU" matokeo yake yako wazi... Akikamatwa hupatiwa maumivu aliyoyakwepa na hata huchoshwa sana. Kiuhalisia inasemekana kuwa mtu yeyote anayeishi anadhulumu kwa kiasi fulani nafsi au vitu vinanvyomzunguka. Kwa mfano hewa tunayovuta huwa tunaigombania na ndio sababu mapafu yetu hupanda na kushuka IKIWA NI ISHARA YA USHINDANI. Kwenye utajiri pia, ili mmoja awe maskini, ni lazima yule aliyetajiri amfanye maskini asiwe na elimu...maarifa na zaidi awe na utiifu kwake...kitu ambacho kinafanya sisi kama jamii tuone sawa japokuwa si sawa na ama hakika Mabadiliko ya lazima yanahitajika haraka kwenye jamii yetu. TATIZO KUU. "KWENYE JAMII YETU KUNA VITU WAMESHAVIKUBALI NA KUONA VIKO

MAMBO 4 YA KUACHA SASA ILI UWE MSHINDI.

 Na, Brightermango. MAMBO 4 YA KUACHA SASA ILI UWE MSHINDI.  1. ACHA KUANDAMANA NA WATU WASIO SAHIHI. Maisha haya ni mafupi kiasi kuwa kama tutaruhusu namna yoyote kuwa na watu ambao muda mwingi wanakurudisha nyuma haiwezi kamwe kuwa sawa au na usaidizi badala yake tutaambulia hasara kubwa. Ishara ya wazi  ya watu hao, mara zote wana kuwa na wewe kwenye muda wako wa juu wa mafanikio lakini ukianza kushuka hutomuona yeyote kati yao.   Anza kuandamana na watu sahihi: hawa ni wale tu ambao wanatambua mchango wako na kuelewa zaidi hata kama hujawaeleza kukuhusu. photo: Employment page. 2. ACHA KUKWEPA AU KUKIMBIA MATATIZO YAKO. Saa chache unapokutana na tatizo huwa unapatwa na hofu... lakini kumbuka kadiri unavyojiimarisha zaidi katika kutatua changamoto ndivyo unavyokomaa kukabili nafasi za juu na kubwa hapo mbeleni aidha kwenye ajira au binafsi. ...Jaribu sasa kupambana nayo; Ukweli ni kwamba hata kama ungepaa juu zaidi na kuishi huko ulikokwenda huwezi kukwepa matatizo yanayokuhusu wewe