Skip to main content

HEKIMA YA MAJI NA MUOGELEAJI.

 HEKIMA YA MAJI NA MWOGELEAJI.



 Wakati wa ajali kutokea kwenye maji, na waokoaji kufikia eneo lile kwa wakati, huwa kuna tahadhari ya Muhimu watu hawa huchukua...

 Yaani kama umezama(drowned) kwenye maji, kwa mara tatu wewe utaenda chini na kurudi juu ndipo utakufa....hivyo wavuvi na waokoaji huwa wana subiri uzame mara mbili na kukutoa kwenye maji:.


SWALI.. KWANINI HUFANYA HIVI.?

Jibu ni kuwa, kipindi unapopambana na maji, kwa kuzama huwa unakunywa maji mengi na hii inatokana na hofu pia kutojua kuogelea, kwahiyo kipindi umezama mara ya kwanza, huwa bado una NGUVU HATA ZA KUWEZA KUMVUTA MTU AU KITU KARIBU YAKO NA HATA KUPELEKEA NA CHENYEWE KUFA... Hivyo wavuvi hukwepa adha ya kupoteza maisha yao kwa kukusubiri uzame mara ya pili na kisha upoteze nguvu... hapo ndipo na wao wanakuja kukuokoa.


FUNZO NI LIPI SASA HAPA?

Funzo liko wazi, kama kweli unampenda mtu kiasi cha kumsaidia, Basi JIHAKIKISHIE KWANZA USALAMA wako kama vile wanavyofanya wavuvi kabla ya kumuokoa mtu majini.

Walio wengi tunasahau, kuwa upendo wa kweli ni Kumpenda mtu yeyote kama tunavyojipenda wenyewe... na kupenda huko ndio hivi, ya kwamba wote tuwe salama kabla na baada ya misaada tunayopeana.


*ANGALIZO*


IKIWA JAMBO UNALITAKA KULIFANYA LITAHATARISHA USALAMA WAKO WEWE, USILIFANYE MPAKA PALE UTAKAPO GUNDUA JINSI YA KUIKWEPA HATARI YAKE.

 

kwa haya na mengine mengi Fuata/follow

Blog yangu ya 

brightermango

Page yangu ya 

Brightermango purpose

Na acount yangu ya 

Brighter Mango

Na jiunge na group langu la facebook 

Jina ni BRIGHTERMANGO.


MUNGU AWABIRIKI NYOTE.

Comments

Popular posts from this blog

UMUHIMU WA NDOTO.

 Brightermango. KILA MTU ATIMIZE NDOTO ZAKE, SIO LAZIMA WOTE WAWE KAMA WEWE.  Inauma  sana pale unapoona mtu au kundi la watu, wanapoenda kinyume na vile ulivyotamani kuwaona. Kila wakati yamkini ukiwaona unahisi kukwazika, SASA SWALI NI KWAMBA, JE? walipaswa kuwa sawa kama ulivyotaka au walipaswa kufuata matamanio yao binafsi, Ukiepusha ushauri wa mtu kuwa mfuasi wa Iman, au Deen, basi mengine yoote ambayo ni matamanio yetu binafsi hayapaswi kurithiwa na watu wengine, haijalishi ni ndugu, rafiki au hata mtoto wako.  WANASEMA, SIKU HIZI mtoto huyu anafuata mambo yake tu, au Rafiki yangu simuelewi kwani siku hizi hafanani na mimi. WAPO WENGI WANATAMANI KUWAFANYA WENGINE KUFANANA NAO, nafikiri ni kosa la kimkakati linalotokea tangu wazazi wetu wanapotuzaa,kututunza, na kutuongoza sisi ambao ni watoto wao. Iwe kheri kwenu nyote, kwamba, Hakuna Tabia(ndoto) iliyo ya lazima kurithi.  Unaweza kufaulu kumfanya mtu kuwa kama wewe kwa kiasi fulani, lakini kukutana changamoto kama zako akanasa n

MAMBO 4 YA KUACHA SASA ILI UWE MSHINDI.

 Na, Brightermango. MAMBO 4 YA KUACHA SASA ILI UWE MSHINDI.  1. ACHA KUANDAMANA NA WATU WASIO SAHIHI. Maisha haya ni mafupi kiasi kuwa kama tutaruhusu namna yoyote kuwa na watu ambao muda mwingi wanakurudisha nyuma haiwezi kamwe kuwa sawa au na usaidizi badala yake tutaambulia hasara kubwa. Ishara ya wazi  ya watu hao, mara zote wana kuwa na wewe kwenye muda wako wa juu wa mafanikio lakini ukianza kushuka hutomuona yeyote kati yao.   Anza kuandamana na watu sahihi: hawa ni wale tu ambao wanatambua mchango wako na kuelewa zaidi hata kama hujawaeleza kukuhusu. photo: Employment page. 2. ACHA KUKWEPA AU KUKIMBIA MATATIZO YAKO. Saa chache unapokutana na tatizo huwa unapatwa na hofu... lakini kumbuka kadiri unavyojiimarisha zaidi katika kutatua changamoto ndivyo unavyokomaa kukabili nafasi za juu na kubwa hapo mbeleni aidha kwenye ajira au binafsi. ...Jaribu sasa kupambana nayo; Ukweli ni kwamba hata kama ungepaa juu zaidi na kuishi huko ulikokwenda huwezi kukwepa matatizo yanayokuhusu wewe

SIRI|| KUFANIKIWA NI KUSUBIRI.

 Na brightermango. VIPI UMEJARIBU KILA KITU LAKINI  BADO TU UNAKWAMA? Hapana, hujajaribu kila kitu, JE? umejaribu kuendelea kusubiri zaidi. Kuna wakati tunatamani mambo yaliyo juu ya upeo wetu, na tukishauriwa mara nyingi tunagundua hatukupaswa kuyatamani na badala yake kutafuta uwezo kwanza wa kuwa pale kama wahusika, yaani ninachokisema ni kwamba; "TUNAPOTAMANI KUWA KWENYE SHEREHE YA KUHITIMU ELIMU YA CHUO, BASI TULIPASWA KUWA WANACHUO AU WAHUSIKA KWA NAMNA FULANI" au "HUWEZI TUNUKIWA MEDANI KAMA HUKUSHIRIKI MASHINDANO HUSIKA" Basi ndivyo ilivyo kwenye maisha, Yaani ukiyahitaji mambo fulani hapa duniani, jitahidi ujue vigezo vyake ili na wewe uweze kuwa kama vigezo vinavyokutaka. Sasa kwenye hili letu la kujaribu kila kitu lakini bado husogei, Je? Ndio haiwezekani tena wewe kuinuka juu na kufanya mambo yako kwa mafakio? Nifuate kuna kitu leo nitakufunza,... NGOJA TUCHIMBE BUSARA ZA MABABU. Kutoka kwenye kitabu cha THE LIFE, Kinachohusika na uandishi wa