Brightermango.
LAU KAMA TUNGEJUA MAISHA NI SAFARI NA NAULI TUNALIPA MWISHO..
Basi tusingechukiana pasipo sababu, wala kusemana (backbitting) hata kama sababu zingekuwepo basi kwa upendo tungeelezana na pasipo chuki tungerekebishana.
IBADA tungefanya kwa uaminifu mkubwa, walio Wakristo, Misingi ya Imani tungeifuata na kukumbushana huku tukiusiana juu ya siku ile ya Mwisho ya Kiama.
KWA MUSLIMS pia tusingekubali kufanya Ibada peke yetu na tungejifunza dini sana ili kwa nafasi zetu tukusanye nauli za kutosha, Maana ni adhabu kubwa kiasi gani kwa anayeitaliki swala, Heri mtu yule aionaye njia ya ibada na kuiendea kuliko yule anayejawa na kibri na ukaidi.
MSAADA; siku zote tungekuwa wa kwanza kuwasaidia wanaotuzunguka kwani tungejua ya kuwa vyoote na yote tulinayo hayatoshi Kulipia SAFARI YETU na hivyo tungetaka nyongeza kwenye mali na kila kitu chetu.
WATOTO YATIMA,Kamwe tusingefurahi kuwepo maneno kama "Watoto wa Mitaani" Ilhari tuko na nafasi na uwezo wa kuwatunza, na zaidi tungeondoa kabisa maeneo ya wao kutunzwa na kuishi nao kwenye majumba yetu.
SAFARI NI SAFARI, Kwa hiyo tusingekubali kubaki nyuma wakati wa kuondoka, na tusingeondoka kama tunahama hivi, bali tungekuwa na wasaa wa kuwapa nafasi zetu wengine waliobaki kwa kuwaelekeza tulivyofanya.
TUSINGE DHULUMU, kama tulivyo waliowengi, huwa tuko bize kuomba punguzo la nauli, kama tungegundua tu kuwa maisha haya ni safari basi tusingeomba punguzo na badala yake tungehitaji zaidi maandalizi ya pesa za kutosha ili tufike salama salimini tukiwa tume keti na tuko tayari.
KUFA, kusingekuwa kitisho chochote kwani tungetambua ya kuwa huo ndio wakati sahihi wa kuondoka ndani ya lile Gari la safari.
JITAFAKARI, BAADA YA KUFIKA HUKO MWISHO, NAULI UNGEKUWA NAYO YA KULIPIA WALAU KWA KIWANGO CHA KAWAIDA NA SIO KILE CHA LUXURY.
Sidhani kama wote tuko tayari kwa Nauli,, ila cha muhimu Turudi nyuma na kujipanga kwa kurekebisha pale tunapohisi tumekwama na hatimae tuvuke au tusafiri kwa amani tukiwa na NAULI ya safari hii ndefu ya hapa Duniani.
Basi tuwausie na wengine kwa kushirikisha andiko hili.
Kwa Tafakuri kama hizi, nifuate/Nifollow.
Mimi
↪Brighter Mango
Page yangu
↪ Brightermango purpose
GROUP NI
↪BRIGHTERMANGO
contact +255747270003.
#SHARE
Comments
Post a Comment