Skip to main content

SIRI|| KUFANIKIWA NI KUSUBIRI.

 Na brightermango.

VIPI UMEJARIBU KILA KITU LAKINI  BADO TU UNAKWAMA?
Hapana, hujajaribu kila kitu, JE? umejaribu kuendelea kusubiri zaidi.
Kuna wakati tunatamani mambo yaliyo juu ya upeo wetu, na tukishauriwa mara nyingi tunagundua hatukupaswa kuyatamani na badala yake kutafuta uwezo kwanza wa kuwa pale kama wahusika, yaani ninachokisema ni kwamba; "TUNAPOTAMANI KUWA KWENYE SHEREHE YA KUHITIMU ELIMU YA CHUO, BASI TULIPASWA KUWA WANACHUO AU WAHUSIKA KWA NAMNA FULANI" au "HUWEZI TUNUKIWA MEDANI KAMA HUKUSHIRIKI MASHINDANO HUSIKA"

Basi ndivyo ilivyo kwenye maisha, Yaani ukiyahitaji mambo fulani hapa duniani, jitahidi ujue vigezo vyake ili na wewe uweze kuwa kama vigezo vinavyokutaka.
Sasa kwenye hili letu la kujaribu kila kitu lakini bado husogei, Je? Ndio haiwezekani tena wewe kuinuka juu na kufanya mambo yako kwa mafakio?
Nifuate kuna kitu leo nitakufunza,...

NGOJA TUCHIMBE BUSARA ZA MABABU.
Kutoka kwenye kitabu cha THE LIFE, Kinachohusika na uandishi wa vitabu vinavyoonyesha maisha ya wazi waliowahi kuishi watu mashuhuri, KILINUKUU KAULI YA   Bruce Lee
"HAKUNA SIRAHA YENYE NGUVU ZAIDI YA NIA",
Akimaanisha #NIA ndio siraha imara kwa ajili ya kila vita kwenye haya, maisha  kwa wasiomjua huyu alikuwa ni mwalimu wa ngumi aina ya #Wingchun na baadae aliboresha staili ile na kugundua staili yake ya ngumi mpya aliyoiita #jeetkundo huku akifanya
Midaharo iliyoruhusu mapambano ya ngumi dhidi ya wale waliobeza elimu yake ya ngumi, pia anakumbukwa kuwa mwanafalsa mwenye upeo mkubwa wa kufanya maamuzi, zaidi ya yote alikuwa muigizaji wa picha za Ngumi, kwa reference nimekuwekea picha hapo chini.

BAADA YA MUNGU SASA LINALOFUATIA NI HILI LA KUTIA #NIA.

#NIA ilimfanya Sr Ramanujan kusafiri kutoka INDIA ya kusini hadi Uingereza akisaidiwa na Mr littlewood ili tu achapishe Andiko lake la hisabati la "Infinte series".
#NIA ilimfanya Adolf hitler akwee mpaka juu na kufanya aliyoyafanya.
#NIA Ndio ilitufungulia dunia ya wireless, kutoka kwa MSERBIA NIKOLA TESLA, ambae baadae sana alihamia marekani na zaidi kugundua Ac motor, na kurahisisha usafirishaji wa umeme kwa haraka zaidi ya ile aliyokuwa anatumia Sir Thomas Edison Alva, pia huyu kaboresha sekta ya ulinzi kwa kugundua nyambizi( torpedo ), Remote controller... pia ndiye aliyeboresha radio wave transmission na mengine mengi.
#NIA Ilimfanya Mahatma kutokuwa na amani mpaka alipowakomboa Wahindi.
#NIA ilimpeleka ikulu Nelson Mandela baada ya zaidi ya miongo kadhaa kwenye mapambano.


CONT.. 0747270003
UNAHITAJI #NIA ILI UFANIKIWE.

Comments

Popular posts from this blog

UMUHIMU WA NDOTO.

 Brightermango. KILA MTU ATIMIZE NDOTO ZAKE, SIO LAZIMA WOTE WAWE KAMA WEWE.  Inauma  sana pale unapoona mtu au kundi la watu, wanapoenda kinyume na vile ulivyotamani kuwaona. Kila wakati yamkini ukiwaona unahisi kukwazika, SASA SWALI NI KWAMBA, JE? walipaswa kuwa sawa kama ulivyotaka au walipaswa kufuata matamanio yao binafsi, Ukiepusha ushauri wa mtu kuwa mfuasi wa Iman, au Deen, basi mengine yoote ambayo ni matamanio yetu binafsi hayapaswi kurithiwa na watu wengine, haijalishi ni ndugu, rafiki au hata mtoto wako.  WANASEMA, SIKU HIZI mtoto huyu anafuata mambo yake tu, au Rafiki yangu simuelewi kwani siku hizi hafanani na mimi. WAPO WENGI WANATAMANI KUWAFANYA WENGINE KUFANANA NAO, nafikiri ni kosa la kimkakati linalotokea tangu wazazi wetu wanapotuzaa,kututunza, na kutuongoza sisi ambao ni watoto wao. Iwe kheri kwenu nyote, kwamba, Hakuna Tabia(ndoto) iliyo ya lazima kurithi.  Unaweza kufaulu kumfanya mtu kuwa kama wewe kwa kiasi fulani, lakini kukutana changamoto kama zako akanasa n

MAMBO 4 YA KUACHA SASA ILI UWE MSHINDI.

 Na, Brightermango. MAMBO 4 YA KUACHA SASA ILI UWE MSHINDI.  1. ACHA KUANDAMANA NA WATU WASIO SAHIHI. Maisha haya ni mafupi kiasi kuwa kama tutaruhusu namna yoyote kuwa na watu ambao muda mwingi wanakurudisha nyuma haiwezi kamwe kuwa sawa au na usaidizi badala yake tutaambulia hasara kubwa. Ishara ya wazi  ya watu hao, mara zote wana kuwa na wewe kwenye muda wako wa juu wa mafanikio lakini ukianza kushuka hutomuona yeyote kati yao.   Anza kuandamana na watu sahihi: hawa ni wale tu ambao wanatambua mchango wako na kuelewa zaidi hata kama hujawaeleza kukuhusu. photo: Employment page. 2. ACHA KUKWEPA AU KUKIMBIA MATATIZO YAKO. Saa chache unapokutana na tatizo huwa unapatwa na hofu... lakini kumbuka kadiri unavyojiimarisha zaidi katika kutatua changamoto ndivyo unavyokomaa kukabili nafasi za juu na kubwa hapo mbeleni aidha kwenye ajira au binafsi. ...Jaribu sasa kupambana nayo; Ukweli ni kwamba hata kama ungepaa juu zaidi na kuishi huko ulikokwenda huwezi kukwepa matatizo yanayokuhusu wewe