Skip to main content

UMUHIMU WA NDOTO.

 Brightermango.

KILA MTU ATIMIZE NDOTO ZAKE, SIO LAZIMA WOTE WAWE KAMA WEWE.

 Inauma  sana pale unapoona mtu au kundi la watu, wanapoenda kinyume na vile ulivyotamani kuwaona. Kila wakati yamkini ukiwaona unahisi kukwazika, SASA SWALI NI KWAMBA, JE? walipaswa kuwa sawa kama ulivyotaka au walipaswa kufuata matamanio yao binafsi, Ukiepusha ushauri wa mtu kuwa mfuasi wa Iman, au Deen, basi mengine yoote ambayo ni matamanio yetu binafsi hayapaswi kurithiwa na watu wengine, haijalishi ni ndugu, rafiki au hata mtoto wako.


 WANASEMA, SIKU HIZI mtoto huyu anafuata mambo yake tu, au Rafiki yangu simuelewi kwani siku hizi hafanani na mimi. WAPO WENGI WANATAMANI KUWAFANYA WENGINE KUFANANA NAO, nafikiri ni kosa la kimkakati linalotokea tangu wazazi wetu wanapotuzaa,kututunza, na kutuongoza sisi ambao ni watoto wao.


Iwe kheri kwenu nyote, kwamba, Hakuna Tabia(ndoto) iliyo ya lazima kurithi. 

Unaweza kufaulu kumfanya mtu kuwa kama wewe kwa kiasi fulani, lakini kukutana changamoto kama zako akanasa na kushindwa kufanikiwa kuikwepa changamoto hiyo.

NA HII NDIO SABABU KWENYE FAMILIA KUNA MMOJA ANA JIHESHIMU NA MWINGINE HAJIHESHIMU.

YUPO yule ana MITUSI MINGI MDOMONI, japo kwao hawatukani na wamejaribu kumnyoosha imeshindikana.


HII ndio sababu ambayo wengi tunatamani kuwabadilisha ndugu zetu, kwa kipindi cha udogo wao wanatutii lakini wakiwa wakubwa wanachukua njia nyingine.

JAPO SIO KOSA, SISEMI KUWA SIO HALALI KUWABADILISHA AU KUWARITHISHA TABIA NJEMA.

ILA UKIONA KAIACHA NJIA, MUACHE AWE NA IKITOKEA KAENDELEA KUFANYA YAKE KWA MAFANIKIO BASI MPONGEZE, ILA KAMA ALIKOSEA NA KURUDI KUJIFUNZA BASI ACHA MLANGO WA MAZUNGUMZO WAZI.

Maana bin adamu Tumeumbwa kujikubali zaidi, Hivyo kuna wakati tunakosea kuyaona mambo mazuri kutoka kwa wale wanaotuzunguka kwa kutaka wao tu wafuate yale tunayotaka peke yetu.

 

USIJEJICHUKIA KWA KUMFANYA AWE VILE ULIVYOTAKA... KUNA WATU WAO NI MIFANO DHAHIRI KUFUATA.Lakini sio kila mtu ni mfano dhahiri wa kufuatwa.


LENGO: MALEZI YAKO YASIZUIE NDOTO ZA WANAOKUZUNGUKA.... Haijalishi kiasi gani unawapenda wanaokuzunguka, changamoto ya kuwafanya wafanye tu mambo unayoyapenda wewe peke yako inawanyima nafasi ya kuwa Huru kifikra.

MFANO: Gaidi huwa anafikiri yuko sahihi kukirithisha kizazi chake ndoto zake na kuwaanda watoto wake wawe kama yeye.

Bila kujali nini watoto wanahitaji, atawafundisha kwa lazima mbinu zake na ikibidi anaweza wauwa wakeze tu kutimiza adhma yake.

"Ila hii iko tofauti tu kwa gaidi mmoja mkolombia aliyeitwa Pablo Escobar."


PHOTO:  URIA PETER.


Comments

Popular posts from this blog

HEY YOU THERE... WHAT ARE YOU WAITING FOR?

It is called liking and not loving... if he could have been loving you...he probably could be doing these.. I mean caring actions would be his song towards you.. and good example is that of flower.. when we pluck it from its pot.. that is showing affection... which may result out of greedy and if you water the flower on its pot.. that means you love them..... are we clear now??